USSD Codes Muhimu za Simu za Mkononi Unazopaswa Kuzijua
Katika dunia ya sasa ya teknolojia ya mawasiliano, kujua USSD codes mbalimbali ni silaha muhimu kwa watumiaji wa simu za mkononi.
Codes hizi husaidia kwa haraka kupata taarifa za kifaa chako, kudhibiti simu zako, na kufanya marekebisho madogo bila msaada wa fundi.
Katika makala hii, tutakuletea orodha kamili ya USSD codes muhimu — kuanzia zile za kuangalia IMEI hadi Call Forwarding na Call Barring.
USSD Codes za Kawaida kwa Taarifa za Simu
USSD codes za kawaida hukusaidia kujua taarifa muhimu kuhusu simu yako bila kutumia intaneti.
Hizi hapa ni codes maarufu unazoweza kutumia:
1.*#06# — Kuangalia IMEI (International Mobile Equipment Identity) ya simu.
2.*#07# — Kuangalia SAR value (kiasi cha mionzi inayotolewa na simu).
3.*#0*# — Kufungua Test Mode (kuangalia screen, vibration, sensors) — inafanya kazi zaidi kwenye Samsung na baadhi ya Android.
4.*#*#4636#*#* — Kuangalia taarifa za Simu, Battery, na Wi-Fi.
5.*#*#7780#*#* — Kufanya Factory Reset bila kureflash firmware (futa data zote za mtumiaji).
6.*#2767*3855# — Kufanya Full Factory Reset (kufuta data zote na kureinstall mfumo wa simu).Hii utakusaidia simu yako ikiwa hacked ufute data zote hata virus ambazo umewekewa.
7.*#*#34971539#*#* — Kuangalia taarifa za kamera ya simu.
8.*#*#232338#*#* — Kuangalia MAC address ya Wi-Fi.
9.*#*#1472365#*#* — Kupima usahihi wa GPS ya simu yako.
10.*#*#2664#*#* — Kupima Touchscreen responsiveness (hali ya kugusa).
11.*#*#0289#*#* — Kupima Audio/Sauti ya simu.
12.*#*#0588#*#* — Kupima Proximity Sensor (sensor inayozima screen unapopiga simu).
13.*#12580*369# — Kuangalia Software na Hardware version ya simu.
USSD Codes za Call Forwarding (Kuhamisha call kutoka sim moja kwenda nyingine)
Call Forwarding hukuwezesha kuhamisha simu zako kwenda kwenye namba nyingine. Hii ni muhimu sana kama hutaki kupoteza simu unapokuwa bize au uko nje ya mtandao.
Hizi hapa ni codes muhimu:
1.*21*namba# — Hamisha simu zote kwa namba nyingine.
2.*61*namba# — Hamisha simu zisizopokelewa (no answer).
3.*62*namba# — Hamisha simu ikiwa imezimwa au uko nje ya mtandao (unreachable).
4.*67*namba# — Hamisha simu ikiwa uko kwenye simu nyingine (busy).
5.##002# — Futa Call Forwarding zote kwenye simu.
Mfano wa kutumia:
Kuhamisha simu zote kwenda kwa namba +255712345678, piga:
*21*+255712345678#
USSD Codes za Call Barring (Kuzuia Simu)
Call Barring hukuwezesha kuzuia simu za kupiga au kupokea, kwa usalama zaidi au kulinda matumizi ya simu.
Hizi hapa codes muhimu:
1.*33*PIN# — Zuia simu zote za kupiga (Outgoing calls barring).
2.#33*PIN# — Ondoa zuio la kupiga simu.
3.*35*PIN# — Zuia simu zote za kupokea (Incoming calls barring).
4.*35*PIN# — Ondoa zuio la kupokea simu.
5.*#33# — Angalia hali ya Call Barring.
Kumbuka: PIN default mara nyingi ni 0000 au 1234, isipokuwa kama umeibadilisha.
USSD Codes za Call Waiting (Simu Kusubiri)
Call Waiting inaruhusu kupokea simu mpya ukiwa kwenye mazungumzo na simu nyingine.
1.*43# — Weka Call Waiting.
2.#43# — Zima Call Waiting.
3.*#43# — Angalia kama Call Waiting ipo hewani
Codes za Kufungua Namba Zilizofungwa: Jua Maana Yake, Hatari Zake na Mbinu za Matapeli
Inawezekana ushakutana na codes hizi ukielezwa zinasaidia kufungua namba iliyofungwa. Lakini kabla ya kutumia, ni muhimu kufahamu kazi yake halisi, na kwa nini matapeli huzitumia kwa ujanja wao. Twende pamoja—usije ukavuruga mambo
Zifuatazo ni Codes Maarufu na Maana Zake
1. #002# – Kufungua Call Barring Zote
Kazi: Inaondoa vizuizi vyote vya simu – kupiga, kupokea na SMS.
Maana: Simu yako inaruhusiwa kufanya shughuli zote bila vizuizi.
Hatari: Ikiwa laini yako ilifungwa kwa uhalifu au usalama, hii inaweza kuruhusu matumizi ya kihalifu kuendelea.
2. #33*0000# – Kufungua Simu za Kuingia (Incoming Calls)
Kazi: Inaruhusu tena kupokea simu zilizozuiwa.
PIN: 0000
3. #33*1111# – Kufungua Incoming Calls kwa PIN Tofauti
Kazi: Sawa na ya juu lakini PIN ni 1111 badala ya 0000.
4. #35*0000# – Kufungua Simu za Kutoka (Outgoing Calls)
Kazi: Hufuta vizuizi vya kupiga simu.
PIN: 0000
5. #35*1111# – Kufungua Outgoing Calls kwa PIN Tofauti
PIN: 1111
6. #330*0000# – Kufungua Vizuizi Vyote (Simu na SMS)
Kazi: Hufuta vizuizi vyote – kupiga, kupokea na SMS.
Hatari: Hii ni hatari zaidi kwani inafuta kila zuio lililowekwa kwa usalama.
PIN: 0000
7. #330*1111# – Kufungua Vizuizi Vyote kwa PIN 1111
Kazi: Kama ya juu, lakini PIN ni 1111.
8. #335*0000# – Kufungua SMS
Kazi: Inaondoa zuio la kutuma au kupokea SMS.
PIN: 0000
9. #333*0000# – Kufungua Intaneti/Data
Kazi: Inaweza kufungua vizuizi vya matumizi ya data/internet.
PIN: 0000
10. #333*1111# – Kufungua Data kwa PIN Tofauti
PIN: 1111
Codes Zilizomalizika kwa 16#
Mfano:
#33*0000*16#
#35*1111*16#
#35*0000*16#
#33*1111*16#
Maana: Codes hizi hufungua vizuizi vinavyohusiana na huduma maalum au kifaa kilichotambuliwa kwa namba 16. Huenda ni voice calls tu, SMS tu au kifaa fulani kama router au modem.
Mbinu Maarufu za Matapeli: Jinsi Wanavyoweka Mtego
Matapeli hawakosi mbinu. Hivi ndivyo wanavyofanya:
Anakupigia kwa namba ya kawaida
Anakujifanya ni mfanyakazi wa kampuni ya simu au TCRA.
Anakwambia kuna "tatizo kwenye laini" yako
Halafu anakushauri upige code fulani “kurekebisha.”
Anakuachia codes
Anakutaka uzipige codes hizo ambazo kwa kweli zinafungua vizuizi kwenye laini yako.
Baadaye anakwambia uwasiliane naye kwa namba nyingine kwa "msaada zaidi"
Hapa ndipo anakuchaji pesa ili kukamilisha huduma – ambayo ni ulaghai mtupu.
Madhara ya Kupiga Codes hizi Bila Kufahamu
Namba yako inaweza kufunguliwa na kurudishwa kwenye matumizi ya kihalifu.
Matapeli wanaweza kutumia laini yako kutapeli watu wengine.
Unaweza kupoteza pesa kwa kulipa kwa huduma hewa.
Ushauri wa Msingi: Jinsi ya Kujilinda
1. Usipige codes bila kujua kazi yake.
2. Wasiliana moja kwa moja na mtoa huduma wako kama namba yako imefungwa.
3. Usilipe pesa kwa mtu binafsi anayejifanya ni msaada wa wateja.
4. Ripoti ulaghai wowote kwa TCRA au kampuni yako ya simu.
5. Tumia namba rasmi pekee za huduma kwa wateja.
Tuchukue Hatua, Tuwashinde Matapeli!
Matapeli wanatumia ujanja mwingi lakini ukielimika huwezi kudanganyika. Usitumie codes hizi bila kuelewa maana yake. Wasiliana na kampuni yako ya simu kwa msaada halali.
Tupinge matapeli – tuache kudanganyika!
Je, umewahi kupigiwa simu ya ulaghai?
Shiriki uzoefu wako hapa chini – tujifunze kwa pamoja!
Tahadhari Unapotumia USSD Codes
Codes zingine zinaweza kufuta data au kurekebisha mfumo wa simu bila onyo.
Hakikisha unaelewa kazi ya code kabla ya kuitumia.
Baadhi ya codes hazifanyi kazi kwenye simu zote; zinaweza kutegemea aina ya simu au mtandao unaotumia.
Kumbuka kuweka backup ya taarifa zako muhimu kabla ya kufanya Factory
Kujua USSD codes hizi ni njia ya kuwa na udhibiti kamili juu ya simu yako bila kutegemea technician au intaneti.
Unaweza kuangalia afya ya kifaa chako, kulinda mawasiliano yako, na kufanya marekebisho rahisi kwa haraka zaidi.
Jifunze, zitumie kwa uangalifu, na endelea kuwa na simu salama!